Kipaji cha mtoto huanza kuonekana taratibu wakati anaendelea kukua, mara nyingi wazazi huwa wanakua wa kwanza zazi ndio wakati wa kutambua mwanaye anataka nini kwa
maisha yake ya baadaye lakini kipaji cha mtoto Esther Okade kimekua cha ajabu na kumshangaza kila mmoja.
Unaweza usiamini lakini huu ni ukweli, Esther ambaye ana umri wa miaka 10 amejiunga na masomo ya chuo kikuu huria cha Uingereza miezi mitatu iliyopita akisomea shahada ya hesabu.
Mtoto huyo ambaye anatokea katika mji wa Walsaw uliopo Midlands, Uingereza sio mtoto pekee mwenye kipaji cha aina yake, mdogo wake wa kiume mwenye miaka sita anasoma masomo ya kidato cha tano katika mchepuo wa hesabu.
Pamoja na Esther kudahiliwa miezi mitatu iliyopita ameonekana kufanya vizuri kuzidi wenzake darasani.
Mama yake Esther aitwaye Ife anasema kitendo cha mwanae kujiunga chuo kikuu kilikuwa la kushangaza kutokana na umri wake kuwa mdogo lakini mwenyewe alijiamini na kuona anaweza.
“Tangu akiwa na miaka saba alikuwa na shauku ya kujiunga na chuo kikuu ili atimize ndoto zake, alikua na kipaji cha aina yake darasani na baada ya miaka mitatu aliuliza tena ikabidi tumpeleke ili kuona kama kweli atamudu“– amenukuliwa Ife, mama wa Esther.
Historia inaonyesha kuwa Esther ni wa kwanza kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri mdogo ingawa mtoto aitwaye Ruth Lawrance alijiunga na chuo kikuu cha Oxford mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 12 na kuhitimu mwaka 1985 (baada ya miaka miwili tu). Baadaye alisoma shahada nyingine ya kwanza ya fizikia kabla ya kusomea PhD ambayo aliimaliza akiwa na umri wa miaka 17. Kwa sasa Ruth ni Profesa wa mahesabu katika chuo Kikuu cha Hebrew Univeristy of Jerusaleem.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni