Leo APRIL
4 2015 historia imeandikwa kwenye michezo TZ, wawakilishi wetu kwenye
Michuano ya Shirikisho la Soka Afrika, Yanga SC wameikamilisha kazi ya
kutuwakilisha uwanjani Zimbabwe ambapo walikuwa wakipambana na timu ya
nchi hiyo FC Platinum kwenye mchezo wa marudiano.
Matokeo ya mechi ya kwanza ambayo ilichezwa TZ kati ya timu hiyo na
Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa goli 5-1 iliwafanya mabingwa hao
kucheza mchezo huu kwa ujasiri mkubwa sana, huku wenzao wakijiongeza
nguvu ya ziada ili wapate matokeo mazuri nyumbani kwao.
Dakika 90
zilikamilika zikaongezwa nyingine nne lakini haikusaidia kubadili
matokeo hayo,FC Platinum walitoka na ushindi wa goli 1-0, lakini matokeo
hayo bado yanaipa nafasiYanga kuendelea na mashindano hayo huku safari
ya Platinum ikiishia hapohapo nyumbani kwao kwenye Uwanja wa Mandav
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni