Rais wa shirikisho la soka Duniani FIFA Sepp Blatter,amekataa kata kata kujiuzulu.
Rais wa shirikisho la soka barani ulaya Michel Platini amewambia waandishi wa habari kuwa Blatter amekataa wito wa kujiuzulu.Platini amesema kuwa kufuatia uamuzi huo UEFA sasa itashiriki uchaguzi hapo kesho na imewashauri washirika wake kumpigia kura mpinzani wa Blatter mwanamfalme Ali bin al-Hussein kutoka Jordan.
Bara la Afrika limeahidi kumpigia kura Blatter sawa na shirikisho la bara Asia.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 anawania nafasi ya kuwa rais wa FIFA kwa kipindi cha tano mfululizo.
Viongozi kadhaa walikuwa wamependekeza kuhairishwa kwa uchaguzi huo huku wengine wakimtaka ajiuzulu ilikuwepo na mwanzo mpya katika FIFA.
Awali ,Blatter aliongoza kikao cha dharura cha wanakamati wakuu wa shirikisho hilo huko Zurich Uswisi.
Kikao hicho kinafuatia hatua ya kukamatwa kwa maafisa 7 wakuu na polisi huko Zurich Uswisi kwa tuhuma za ufisadi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni