Jumatano, 3 Juni 2015

BREAKING NEWS SEPP BLATTER AJIUZULU URAIS WA FIFA

Sepp Blatter resigns as FIFA president amid bribery scandal

Sepp Blatter amejiuzulu rasmi urais wa FIFA kufuatia tuhuma za rushwa zinazokabili taasisi hiyo ambayo ndiyo kubwa zaidi duniani inayosimamia soka. Katika hatua inayoshangaza kutoka makao makuu ya FIFA mjini  Zurich nchini Uswisi  Blatter alisisitiza kuwa anaondoka katika hilo baada ya kulitumikia shirika hilo kwa miaka 17 akiwa kiongozi mwenye nguvu zaidi katika masuala ya soka. Blatter kwa sasa anakabiliwa na uchumguzi maalumu kutoka katika shirika la upelelezi la Marekani FBI ambalo linachunguza kama rushwa hizo ziliruhusiwa na Blatter na timu yake ya uongozi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni