Ijumaa, 26 Juni 2015

MTO MFUPI ZAIDI DUNIANI

Kulingana na kitabu cha World Guinness Book of Records mto mfupi zaidi duniani ni mto Roe ambao uko kati ya Giant Springs na Mto Missouri katika (Maanguko Makubwa ya Maji The Great Falls), iliyopo katika jimbo la Montana, nchini Marekani. Mto Roe una urefu wa futi 201 sawa na mita 61. Kuelekea mwishoni mto Roe una kina cha kushangaza cha futi 6–8.

Kable ya hapo mto ulioonekana kuwa mfupi zaidi ulikuwa hukohuko Marekani ni mto D ulioko Oregon Marekani wenye urefu wa futi 440 sawa na mita134. Sifa hii imetenguliwa mwaka 1989.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni