Wengi
wetu tumejikuta katika kizungumkuti hiki, ni ushindani wa kila siku
kuhakikisha kwamba simu ya mkononi ina moto wa kutosha na tunakerwa kila
betri inapopungua nguvu.
Zamani hali ilikuwa tofauti, simu zilitumika kwa mazungumzo tu na ilikuwa rahisi kwa betri kusalia na nguvu kwa muda mrefu.Huenda simu zilikuwa nzito wakati huo mithili ya tofali lakini ni kweli pia kuwa nguvu za betri zilikuwa zinaweza kumudu kwa siku tatu hadi wiki moja.
Lakini sasa imekuwa mtihani wakati tunaona watu waking'ang'ana kufikia soketi za umeme ili kuongeza nguvu simu zao kila wanapoziona.
Taswira huwa za kustaajabisha, wengine wamesimama katika uwanja wa ndege wengine wakichowa baa wanaomba kuchaji simu zao.
Hamu hii kubwa inatokana na kuongezeka matumizi ya simu aina ya smartphones zilizo na apps, ambazo hutumia nguvu nyingi za betri za simu.
Katika nchi kama Rwanda, ambako kunashuhudiwa ongezeko kubwa la matumizi ya simu za mkononi, ni muhimu kuweza kuchaji simu hizo kila wakati.
Mbinu mpya kote duniani zinasaidia watu kuweza kuhifadhi nguvu za betri katika simu zao kwa muda mrefu - jambo ambalo linazidi kuwa muhimu katika dunia ambapo watu wengi wanaathirika na kuwa na wasiwasi kila wanapokuwa mbali na simu zao.
Hali hii inayojulikana kama - Nomophobia. Neno hili lietengenezwa mwaka 2010 kutokana na "no-mobile-phone phobia", kufuatia utafiti uliofanywa UK Post Office
Utafiti kutoka chuo kikuu cha Missouri unadhihirisha uhusiano huu unaongeza viwango vya msongo wa mawazo na kusababisha matatizo makubwa ya akili.
Pamoja na simu zenyewe, kuna biashara kamili iliyoanzishwa sasa ya kuwa na vifaa vya kuongeza nguvu betri za simu maarufu zinazojulikana kama Power bank, ilimradi tu unakumbuka kuvichaji pia vifaa vyenyewe. Wengine wanakuwa na betri mbili au zaidi na kadhalika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni