Kutokana
na hali hiyo kumekuwa na shinikizo kutoka katika makundi mbalimbali
chama hicho kuwa makini kumteua mgombea anayekubalika, msafi na mwenye
kuchagulika ambaye atatoa ushindani kwa wagombea wa upinzani, hasa
UKAWA.
Vilevile,
kumekuwapo na wasiwasi wa baadhi ya wagombea kutishia kukihama chama
hicho endapo majina yao yatakatwa, jambo ambalo pia linakiweka njia
panda.
Nape: Hakuna shinikizo
Hata
hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amejibu hoja hizo
akisema chama hicho hakitafanya uamuzi kwa kushinikizwa na watu, bali
kitafuata taratibu na kanuni.
“Tunazo
taratibu, tunazo kanuni zetu. Nataka kuamini kuwa kila mtu aliyegombea
anajua kuna kushinda na kuna kushindwa na kuna kuteuliwa na
kutokuteuliwa,” alisema jana alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema hataki kuamini kuwa kuna mgombea kati ya 38 walioomba nafasi hiyo ambaye anaamini anaingia kushinda tu.
“Usipokuwa
wewe anakuwa mwingine... Asiyekubali kushindwa basi atakuwa si
mshindani. Usisahau hizo ni presha za wapambe hazitupi tabu. Tunachojua
walioshindwa watapeana mkono na aliyeshinda na chama kitabaki kuwa
kimoja,” alisema Nape.
Alisema wananchi waamini chama kitatenda haki, taratibu zitafuatwa na kuwapa mgombea bora.
“Haya ni
maneno ya presha za barabarani ninachoamini mwisho wa siku hakuna fujo,
hakuna vurugu, vyombo vimejipanga vizuri hakuna vurugu na wapambe
kusindikizana ni jambo la kawaida,” alisema na kuongeza kuwa anafahamu
kuwa wapo watakaohuzunika kutokana na majina ya watu wao kukatwa lakini
hakuna jinsi kwa sababu kanuni za CCM zinasema Kamati Kuu (CC)
itapendekeza majina matano kwa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Pia kanuni hizo zinasema NEC itapendekeza majina matatu kwa mkutano mkuu ambao utachagua mmoja - MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni