Ijumaa, 10 Julai 2015

SANAMU KUBWA YA BILL COSBY YAONDOSHWA DISNEY

 


Mchekeshaji maarufu Marekani Bill Cosby

Sanamu ya mwigizaji Bill Cosby imetolewa katika bustani ya Disney kutokana na kesi inayoendelea kortini ambapo kumetokezea ushahidi kuwa Cosby alikiri kumpatia mwanamke dawa za kulevya kabla ashiriki naye ngono.
Sanamu hii ni moja ya maonyesho katika bustani ya Disney Hollywood, mjini Florida ya kuwatambua waigizaji maarufu .
Nyaraka zilizofichuliwa kortini zinaonyesha kuwa Cosby alitoa ushahidi 2005 kuwa alinunua dawa aina ya Quaaludes kwa madhumuni ya kuwapa wanawake aliotaka kushiriki nao ngono
Cosby anakabiliwa na tuhuma nyingi za unyanyasaji wa kingono kwa miongo kadhaa iliyopita.
Bill mwenye miaka 77, amekataa mashtaka hayo na pia hajawahi kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu.
Kwa sasa, kuna mapendekezo heshima zote alizotonukiwa Cosby zifutiliwe mbali miongoni mwao ni mchoro katika ukuta wa mgahawa mmoja mjini Washington DC, alikozoea kwenda kula.
Wasanii wengi wametoa maoni yao kuhusu ushahidi unaoendelea kujitokeza, wengine wakimuunga mkono kwa matumaini ya kesi kutupiliwa mbali na wengine wakikata uhusiano naye.
''Mshukliwa ni mshukiwa hadi atakapopatikana na hatia'' amesema Whoopi Goldberg.
Mwimbaji Jill Scott aliyekuwa shabiki wake Cosby, katika Twitter amesema ''amechukizwa'' na kwamba ushahidi wake Cosby ''ni hakikisho kuwa alitenda maovu''.

Kuondolewa kwa sanamu ya Cosby katika bustani ya studio za Disney, ni hatua inayofuata malalamiko yaliowasilishwa katika matandao wa Change.org lililosema kwamba sanamu hiyo haifai kuwepo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni