Rais wa zamani wa Marekani
Jimmy Carter ametangaza kuwa ana maradhi ya saratani.
Carter mwenye umri wa
miaka tisini, na siku za hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa ini.
Jimmy amesema kuwa imebainika kuwa ana saratani ambayo imekwisha sambaa katika baadhi ya sehemu za mwili wake.
Ameongeza kuwa yupo katika mpango wa kuweka vizuri ratiba yake kwa lengo la kupata matibabu zaidi.
Jimmy Carter toka aondoke madarakani ,amekua akijisughulisha na kazi za kuhudumia jamii duniani kote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni