Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Nderakindo Kessy
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu
ya chama hicho, Ilala Dar es Salaam jana, wakati akitangaza majimbo
yaliyochini ya vyama vinavyounda Ukawa ambayo vyama hivyo vitasimamisha
wagombea wao katika uchaguzi mkuu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama
cha NLD, Masudi Makunjunga.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Shaweji Mketo (wa
pili kulia), akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari.
Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Masudi
Makunjunga, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Nderakindo
Kessy na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), John Mnyika.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, akizungumza katika mkutano huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni