Jumatatu, 25 Januari 2016

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam wakati alipotangazia umma wa watanzania kuhusu hatua ambazo Rais Dk. John Pombe Magufuli amechukua dhidi ya Dickson Mwaimu  Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho vya taifa NIDA kutengua uteuzi wake na kumsimamisha kazi mara moja pamoja na wasaidizi wake ambao ni Joseph Makani Mkurugenzi wa TEHAM, Bi. Rahel Mapande Afisa Ugavi Mkuu Bi. Sabrina Nyoni Mkurugenzi wa Sheria na George Ntalima Afisa Usafirishaji kwa kuwasimamisha kazi mara moja kupisha uchunguzi.Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia shilingi Bilioni 179.6 kiasi hicho ni kikubwa na Rais angependa kufanyika uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizo zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kazi ndogo ya utoaji wa vitambulisha vya taifa .

Hivyo Rais ameelekeza mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya Umma PPRA wafanye ukaguzi wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA, TAKUKURU na CAG kufanya uchunguzi kwa pamoja ili kubaini kama kulikuwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu au la.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-IKULU)
3
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU Bw. Gerson Msigwa.
4
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiangalia wakati Kaimu mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano IKULU Bw. Gerson Msigwa alipomruhusu mmoja wa waandishi wa habari kuuliza swali katika mkutano huo Ikulu jijini Dar es salaam.
6
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikitolewa na Balozi Ombeni Sefue Ikulu jana.
7
Mkutano ukiendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni