Jumatano, 23 Machi 2016

Ndugu waliojilipua Brussels watambuliwa

 Wawili
Wawili hao, waliovalia jaketi nyeusi, walifariki
Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga waliojilipua katika uwanja wa ndege wa Brussels Jumanne wametambuliwa kuwa ndugu wawili, Khalid na Brahim el-Bakraoui.
Kituo cha runinga cha RTBF kimesema wawili hao walifahamika vyema na polisi.

Mwanamume wa tatu aliyeonekana kwenye video za kamera za siri uwanja wa ndege akiwa pamoja na wawili hao bado anasakwa.
Milipuko miwili ilitokea katika uwanja wa ndege na mwingine mmoja katika kituo cha treni na kuua watu 34 na kujeruhi wengine 250.
Ubelgiji imeanza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
RTBF imesema ndugu hao wawili walifahamika na polisi na wana rekodi za uhalifu lakini hawakudhaniwa kuwa na uhusiano na ugaidi awali.
 
Kumbuka
Hafla za kuwakumbuka waliofariki zimefanyika miji mingi Ulaya
Kituo hicho cha runinga kimesema Khalid el-Bakraoui alitumia jina bandia kukodi nyumba katika eneo la Forest jijini Brussels ambapo polisi walimuua mtu mwenye silaha kwenye makabiliano wiki iliyopita.
Ilikuwa ni wakati wa msako huo ambapo polisi walipata alama za vidole za Salah Abdeslam, mshukiwa mkuu wa mashambulio ya Paris ya 13 Novemba.
Abdesalam alikamatwa kwenye operesheni ya maafisa wa usalama Ijumaa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni