Hofu ya kuwepo bomu uwanjani imesababisha mechi ya Manchester United na Bournemouth kuahirishwa.
Mechi ya mwisho
katika ligi ya soka ya uingereza, EPL, kati ya Manchester united na
Bournemouth imeahairishwa kufuatia wasiwasi wa bomu, uwanjani Old
Trafford.
Kifurushi kinachoshukiwa kuwa na vilipuzi kilipatikana kimetegwa katika sehemu ya North West Quadrant.
Wachezaji wakiongozwa na kocha Louis Van Gaal walirudi kwenye chumba cha mabadiliko.
Tayari kikosi cha timu hiyo kilikuwa kinajiandaa kuingia uwanjani baada ya kutajwa. Maelfu ya mashabiki waliokuwa wanasubiri mchuano huo walilazimika kutoka nje.
Manchester United inashikilia nafasi ya saba ikiwa na alama 63 baada ya mechi 37. Awali Mashabiki wa klabu walionyesha kughadhabishwa na utendakazi wa kocha Van Gaal, wakitaka aachishwe kazi.
Hii ni baada ya Westham kuzamisha matumaini ya klabu hiyo kwa kuizaba 3-2 wiki iliyopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni