Mahakama ya katiba
ya Italia imetoa hukumu dhidi ya sheria inayompatia moja kwa moja mtoto
anayezaliwa ndani ya ndoa jina la baba yake.
Mawakili walidai kuwa kuzuwia familia kuwapatia watoto wao majina ya babu zao wazaa mama ni ubaguzi dhidi ya wanawake.Awali mahakama ya Muungano wa Ulaya ya masuala ya haki za binadamu (ECHR) ililaani sheria hiyo ambayo ilibuniwa tangu enzi za utawala wa waroma - na kuiagiza Italia iibadirishe.
Wanaharakati wamepongeza uamuzi huo uliotolewa Jumanne na kulitaka bunge liidhinishe uamuzi huo.
"mahakama imetangaza kubatilisha kisheria kanuni ambazo zinatoa mamlaka ya moja kwa moja ya kuwaita waototo majina ya ya upande wa familia za baba zao kwa watoto halali, pale ambapo wazazi watakuwa na utashi mwingine ," Ilieleza taarifa ya mahakama ya kikatiba.
Kesi hiyo inahusisha wanandoa, mmoja mtaliano na mwingine mbrazili waliotaka kumpatia mtoto wao wa kiume majina ya yote mawili ya baba zao ,kama ilivyo katika tamaduni za nchi nyingi za kilatino.
Baada ya ombi lao kukataliwa na mamlaka za Italia , waliamua kupeleka kesi yao katika mahakama ya Muungano wa Ulaya ECHR, iliyokubali ombi lao mwaka 2014.
Ilisema kuwa sheria hiyo iko sambamba na sheria na kanuni juu ya usawa wa jinsia unaosisitizwa katika katiba ya sasa ya Italia.
Bunge dogo la Italia limeidhinisha muswada unaolenga kubadili sheria hiyo, lakini umekwamishwa na bunge Seneti kwa miaka kadhaa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni