Ijumaa, 27 Januari 2017

Albright asema ''yuko tayari kuingia usajili ya Waislamu''

Madeleine Albright asema atajisajili kuwa Muislamu iwapo Trump ataanzisha sajili ya Waislamu Marekani

  Madeleine Albright asema atajisajili kuwa Muislamu iwapo Trump ataanzisha usajili wa Waislamu Marekani
Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani na msanii wa Bing bang wameapa kujisajili kama Waislamu iwapo Donald Trump ataanzisha sajili ya waislamu pekee.
Mwanasiasa Madeleine Albright na Mayim Bialik walisema kuwa wako tayari kujisajili kuwa wafuasi wa dini hiyo ili kupinga hatua hiyo ya Trump.
''Nililewa kama Mkatoliki , nikawa Episcopalian na baadaye nikabaini kwamba familia yangu ilikuwa ya Kiyahudi'', Bi Albright, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani alisema katika mtandao wake wa Twitter.
Chapisho hilo lilipendwa na maelfu ya watu.
Tamko lake lilijiri huku kukiwa na uvumi kuhusu agizo la rais ambalo litafanya ukaguzi wa kina, kupiga marufuku wakimbizi mbali na watu wanaoingia kutoka nchini humo kutoka mataifa saba ambayo yatashirikisha Syria,Yemen na Iraq.
Lakini hakujakuwa na usajili wa Wamarekani Waislamu katika miezi ya hivi karibuni, swala ambalo bwana Trump alisema atalitekeleza katika mahojiano mwaka 2015 kabla ya kukana kufanya hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni