Mvumbuzi mmoja wa
Ghana ameonyesha kile anachotaja kuwa uvumbuzi wake wa hivi karibuni
unaoshirikisha magari katika maonyesho ya Kiteknolojia katika mji mkuu
wa Accra.
Kwadwo Sarfo ,mwanzilishi wa taasisi ya kiteknolojia ya
Katanka na mbaye pia ni kiongozi wa dini alionyesha gari alilotengeza
aina ya V8, pikipiki za magurudumu matatu, mashine za roboti za
kuchomelea vyuma miongoni mwa vinginevyo.Rais Nana Akofu-Addo, ambaye alihudhuria maonyesho hayo amesema serikali yake itaangazia kuhusu elimu ya sayansi na teknolojia ili kuimarisha maendeleo ya serikali kulingana na chombo cha habari cha Joy News.
Bw Sarfo ambaye ni babake mbunge mmoja amesema kuwa uvumbuzi wake unaonyesha uwezo mkubwa wa mtu mweusi katika sekta ya teknolojia na uvumbuzi.
Alitengeza gari lake la kwanza mwaka 1998 na tangu wakati huo chapa yake ya Kantanka imetoa magari kadhaa ikiwemo magari yenye magurudumu manne na SUV.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni