Mbunge mmoja ametoa
wito kwa wanawake waliopo katika maeneo yenye wafuasi wengi wa upinzani
nchini Kenya kutofanya mapenzi na waume zao ambao hawajajiandikisha kuwa
wapiga kura.
Kulingana na gazeti la The Standard nchini humo,
mwakilishi wa wanawake mjini Mombasa Mishi Mboko amewataka wanawake
nchini humo kuwanyima wanaume zao haki zao za ndoa ili kuwashinikiza
waende kujiandikisha kuwa wapiga kura ili kujiandaa kwa uchaguzi wa mkuu
ujao unaofanyika tarehe 8 mwezi Agosti 2017.Akizungumza katika uwanja wa maonesho ya kilimo katika eneo la Mkomani Bi Mboko alisema kuwa ngono ni kifaa kizuri kinachoweza kuwashinikiza wanaume kukimbilia kujiandikisha katika shughuli hiyo ilioanza siku ya Jumatatu.
Kulingana na gazeti hilo hata hivyo, mumewe Mboko hatonyimwa haki hiyo ya ndoa kwa kuwa tayari amejiandikisha kuwa mpiga kura.
''Wanawake huu ndio mpango munaofaa kuutumia.Ni mpango muziri sana.Wanyimeni haki yao ya kufanya mapenzi hadi pale watakapowaonyesha cheti cha kupiga kura'', alisema.
Mboko aliongezea kwamba imefikia wakati ambapo wanawake wanafaa kutumia ngono kuwalazimisha waume zao kuchukulia shughuli ya usajili wa wapiga kura na umuhimu mkubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni