Picha ya binti
mfalme Charlotte imetolewa na Kensington Palace kuadhimisha siku yake ya
kuzaliwa anapotimia umri wa miaka miwili siku ya Jumanne.
Picha hiyo aliyochukuliwa na mama yake, inamuonyesha Charlotte nyumbani mwa familia.Familia ilitoa picha ya Charlotte sawa na hiyo mwaka uliopita alipotimia umri wa mwaka mmoja.
Kensington Palace ilisema kuwa kila mmoja anafurahia picha hiyo vile wao wenyewe wanavyoifurahia.
Familia inatarajiwa kumuandalia karamu binti mfalme huyo.
Familia huzuia binti mfalme huyo kuonekana kwa umma lakini alipigwa picha wakati wa ibada ya krismasi katika kijiji cha Bucklebury.
Pia alionekana wakati familia ilifanya ziara nchini Canada ambapo alionekana mara kadha ikiwemo waki wa karamu ya watoto huko Victoria
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni