Jumanne, 2 Mei 2017

Marehemu achoma moto chumba cha kuchomea maiti Marekani

Chumba cha kuchomea mfu huko Ohio Marekani

 Chumba cha kuchomea mfu huko Ohio Marekani
Chumba cha kuchomea maiti katika jimbo la Ohio nchini Marekani kiliungua wakati kilipokuwa kikitumika kuchoma mwili wa mfu aliyenenepa kupita kiasi kulingana na mmiliki wa chumba hicho.
Don Catchen alisema kuwa maiti hiyo ilisababisha moto uliochoma chumba hicho katika mji wa Cincinati.
Mafuta yaliokuwa katika mwili huo yalichomeka katika viwango vya juu vya joto na kusababisha moto huo kulingana na afisa mkuu wa zima moto.
Hata hivyo hakuna eneo jingine la chumba hicho lililochomeka kulingana na Catchen.

Moto huo hatahivyo ulidhibitiwa katika eneo la kutengeza magari ambapo chumba hicho cha kuchomea maiti kipo,aliambia BBC.
Chumba hicho kipo katika mji wa Cincinati. 
Chumba hicho kipo katika mji wa Cincinati.
''Mfanyakazi wangu alikuwa katika kazi ya kuchoma mwili mmoja wa mtu aliyenenepa kupitia kiasi na moto ukawa mkubwa zaidi ya kiwango kinachohitajika''.
"Mojawapo ya makasha ya kuchoma miili liliungua na ni hilo ndilo lililochomwa pekee. Hakuna miili mingine iliyoharibika katika moto huo'',alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni