
Watu 22 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Polisi katika mji
wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 22 wameuawa na wengine 60
kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la
muziki.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi. Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.

Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.


Barabara ya ukumbi huo unuangana na kituoacha treni cha Victoria kati kati mwa mji.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni