Wanajeshi wa
Ubelgiji wamemuua kwa kumpiga risasi mlipuaji wa bomu wa kujitoa
muhanga, katika kituo kikuu cha reli mjini Brussels.
Idara ya
polisi imesema kuwa mtu huyo alikuwa amevalia kile kilichoonekana kuwa
mkanda wa vilipuzi na kuwa kulitokea mlipuko mdogo.Waendesha mashtaka wanasema kuwa mshukiwa huyo amefariki.
Watu waliokuwa katika kituo Kikuu cha mabasi mjini Brussels na eneo la karibu la mnara ambalo hufurika watalii wote waliondolewa.
Wanajeshi wamekuwa wakilinda doria mjini Brussels tangu kulipotokea shambulio la kujitoa mhanga katika eneo la Uwanja wa ndege na kwenye mfumo wa usafiri wa chini ya ardhi mwaka uliopita .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni