Maryam Mirzakhani, mwanamke wa kwanza kushinda tuzo la hesabu la Fields Medal amefariki nchini Marekani.
Professor
Mirzakhan mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni professor katika chuo cha
Stanford, alikuwa akiugua ugonjwa wa Saratani ya matiti ambayo ilisambaa
hadi kwa mifupa yake.Alipewa jina mshindi wa Nobel ya hesabu. Tuzo la Fields Medal hutolewa baada ya kila miaka minne kwa kati wa wasomi wa hesabu wawili na wanne walio chini ya miaka 40.
Rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa kifo cha Prof Mirzakhan kileta huzuni nyingi.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mohammad Javad Zarif, alisem kuwa kifo chake kimewaletea majonzi watu wote nchini iran.
Prof Mirzakhani na mumewe ambaye na mwanasayansi raia wa Czech, wana mtoto mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni