Wakati ulimwengu ulipoadhimisha siku ya idadia ya watu duniani mwanamume mmoja alikuwa na sababu 100 za kusherehekea.
Kofi Asilenu mwenye umri wa miaka 80 ni baba wa watoto 100 na wake 12.Anaishi na familia yake katika kijiji chaAmankrom kilicho umbali wa kilomita 45 kutoka mji mkuu Accra.
Familia yake ni thuluthi moja ya watu 600 katika kijiji hicho.
Anasema kuwa anataka familia kubwa kwa sababu hakuwa na ndugu.
Sina kaka, dada wala shangazi, ndio sababu niliamua kuwa na watoto wengi ndio wapate kunipa maziko yaliyo mazuri nikifa.
Familia hiyo yake hata hivyo imemgharimu pakubwa. anasema alikuwa mtu mwenye mali nyingi, lakini mali hiyo ilipungua sana kutokana na gharama ya kuitunza familia yake kuwa kubwa mno.
Kofi Asilenu anaonekama kuwa mwenye afya nzuri na hata anasema kuwa anataka kupata watoto zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni