Kopo
Mwanamume mmoja amefanikiwa kusafiri na kopo la bia pekee kama mzigo nchini Australia.
Mwanamume huyo ambaye alitambuliwa kama Dean Stinson alisema kuwa rafiki yake alikuwa amependekeza hilo kama mzaha.Kopo hilo lilifika likiwa na kibandiko na likiwa bado halijafunguliwa kama mzigo wa kwanza katika uwanja wa Perth baada ya safari ya saa nne kutoka Melbourne.
Shirika la ndege la Qantas lilisema kuwa haliwashauri abiria wengine kufuata mkondo huo.
Bwana Stinson aliiambia AFP kuwa alifurahi kuwa kopo hio liliwasila salama siku ya Jumamosi.
Shirika hilo halilipishi mizigo ambayo hubebwa na abiria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni