
Jamii ya Wahadzabe
ni moja kati ya makabila yaliyobaki duniani yanayoendeleza shughuli za
uwindaji, inadhaniwa kuwa jamii hii imeishi kaskazini mwa Tanzania,
ikila matunda na mizizi, na aina mbalimbali za wanyama kwa miaka 40,000.
Mwandishi
wa BBC, Dan Saladino alikwenda kuwashuhudia wakikusanya na kuwinda, na
kuchunguza iwapo lishe yao ni suluhu kwa matatizo mengi yanayowasibu
binadamu kwa sasa.Angalizo: Baadhi ya picha ni za wanyama waliouawa ni huenda zikawa za kuogofya.
Wakati nikiwa nimelala kifudifudi, niliweka kichwa changu ndani ya shimo lenye giza nikahisi harufu ya mnyama
Lakini sikuamini kuwa mtu ataingia mle ndani na kumtoa mnyama huyo. Mtu huyo ni Zigwadzee, na mnyama alikuwa nungunungu, amini usiamini.
Baada ya kukabidhi uta, mshale na shoka lake kwa mwindaji mwenzake wa Kihadzabe, Zigwadzee alishika fimbo fupi iliyochongoka na akaingia shimoni.

Hadi hivi sasa chakula changu kutoka jamii ya Wahadzabe kilikuwa ni mboga za majani na matunda tuu. Matunda mengi tuliyachuma katika msitu na vichaka maeneo ya nyika, juu ya miiba na kupitia maeneo yenye nyasi kavu. Wakati mwingine, tungechimbua mizizi kutoka ardhini na kuipika upesi.


Maeneo yote yaliyotuzunguka yalikuwa yamesheheni vyakula lakini sisi hatukuweza kuvitambua lakini hata watoto wadogo katika jamii ya wahadzabe waliweza kutambua na kupata chakula.

Baada ya dakika 40, alijitokeza tena akiwa amejaa vumbi mwilini na viroboto kadhaa, tayari kuchimba chini ya ardhi katika mahali ambapo sasa nungunungu huyo alikuwepo.

Jamii hii inawaona wakulima kama wa kushangaza. Mmoja aliniuliza ''kwa nini kusimama shambani siku nzima na kisha kusubiri chakula kwa majuma na miezi wakati unaweza kula matunda ya msituni, kurina asali nyingi ya kula, au kutumia saa moja kufika yalipo maficho ya nungunungu ukalisha familia nzima?"

Hii ndio namna ambavyo mababu zetu walivyokuwa wakijitafutia chakula.
Vyakula ambavyo Zigwadzee na Wahadzabe wenzake hula ndivyo pekee vilivyosalia vyenye uhusiano na vyakula ambavyo mwili wa binadamu ulibadilika na kuvizoea na ndivyo ambavyo vinaufaa mfumo wetu wa kumeng'enya chakula - ikiwa ni pamoja na bakteria ambao sote tunao tumboni na mfumo wa vijidudu vya kinga dhidi ya maradhi viitwavyo kitaalamu Microbiome. Hivi vina uzani wa kilo moja hadi mbili hivi.
Kumekuwa na hali ya kukubaliana katika ulimwengu wa kitabibu kuwa vijidudu hivyo vina kazi kubwa ya kufanya katika mfumo wa kinga, na kuwa kadiri unapokuwa na bakteria hao kwa wingi, hatari ya kupata maradhi hupungua.
Hali kadhalika kwa Wahadzabe, kutokana na aina ya vyakula wanavyokula, wana vijidudu vya aina nyingi sana vya kinga.



Hivyo alichukua sampuli ya haja kubwa kabla na baada ya siku tatu alipokuwa akila vyakula vya jamii ya Wahadzabe ili kuona kama aina ya vijidudu vinavyosaidia kinga mwilini viliongezeka tumboni mwake.
Matokeo yalikuwa ya kufurahisha. Baada ya siku tatu, aina ya bakteria aliokuwa nao tumboni iliongezeka kwa kiasi cha asilimia 20, na aliweza kugundua aina nadra sana ya bakteria ambao huhusishwa na afya njema mwilini mwake.

Lakini kuna hali ya dharura kiasi, kwa sababu mambo yanabadilika haraka katika maisha ya jamii ya wahadzabe.
Kwa miaka mingi, wakulima wamekuwa wakilima mpaka kuingia maeneo ya ardhi ya Wahadzabe. Katika muongo mmoja uliopita, walikuwa wanafyreka ekari 395 kila mwaka, eneo ambalo Wahadzabe hulitumia kupata chakula.
Wafugaji na ng'ombe wao wenye njaa pia wamekuwa wakiwasili kwa wingi, na kuwafanya wanyama mwitu aina 30 hivi katika maeneo hayo ambao watu wa Wahadzabe wamekuwa wakiwinda na kuwala kwa miaka mingi kutoroka.

Kwangu hata hivyo, kuna jambo jingine lililonishangaza zaidi.
Baada ya kuendesha gari kwa dakika 30 hivi kutoka pahala ambapo tulikuwa tumewinda nungunungu, tulipata nyumba iliyojengwa kwa matope na humo ndani mlikuwa na chupa na mikebe iliyokuwa na soda na pakiti za biskuti. Ilikuwa imenuchukua saa tisa kwa gari aina ya Land Rover kufika hapo, lakini nikapata bidhaa hizo zilikuwa zimenitangulia.

Ana kwa ana na mnyama, Zigwadzee alimgusa gusa na fimbo huku akimuita ''njoo nungunungu...njoo kwangu...njoo hapa nungu nungu! Kisha, si nungunungu mmoja, mbali walitokea wawili.
Kilichoshangaza zaidi si miiba ya wanjama hao - ambao walikuwa wakubwa sana, wa uzani wa kilo 30 kila mmoja - mbali ilikuwa kelele. Miiba iliinuliwa kwa pamoja na kutoa sauti kali. Zigwadzee aliwagonga nungunungu hao vichwani na muda mfupi baadaye, walikuwa wamekufa.

Wawindaji wa Wahadzabe hugawana kila kitu.
Ni jamii yenye usawa.
Hakuna mifumo ya uongozi na kuhusu nyama, hasa, inapopatikana ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha amegawana na wenzake kwa usalama.
Matumbo, moyo, maini na mapafu yalipikwa papo hapo na kuliwa, lakini nyama hiyo nyingine ilisafirishwa hadi kambini na wakagawana.
Nilipowatazama, huku nikiendelea kula kipande changu cha ini la nungunungu, nilitazama jambo la kipekee. Windo, na chakula, ambavyo viliniwezesha kuwa na uhusiano na utamaduni wa kale sana.
Picha zote kwa hisani ya Jeff Leach, chuo kikuu cha King's College London
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni