Alhamisi, 16 Aprili 2015

MAYWEATHER JR AJIFUA KIROHO MBAYA

 

Bondia Floyd Mayweather amesema atapigana mara moja zaidi baada ya kupambana na Manny Pacquiao mwezi ujao, kwa sababu amesema hajisikii kuufurahia tena mchezo wa ndondi.
Mpambano wa Mayweather dhidi ya Pacquiao wa Mei 2 ni wa tano kati ya mapambano sita kwenye mkataba alioingia na shirika la utangazaji la Showtime
Mayweather, 38, amesema ile "furaha" haipo tena kwenye ndondi, na sasa anatazama fani hiyo kama "kazi" tu.
Amesema: "Sifurahii sana kama ilivyokuwa zamani. Pigano langu la mwisho ni Septemba."








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni