Je unampenda paka ?
Awe
ni paka wa nyumbani ama yule paka wa pori na wanyama wote katika
jamii ya paka kama vile simba, ama chui, paka huvutia hisia nyingi sana
kwa mwanadamu.Lakini mapenzi hayo ya paka yamefikia hatu mpya.
Amini usiamini ofisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.
Paka hmmoja ambaye zamani alinusuriwa alipokuwa akizurura mitaani katika mji mkuu wa London -- alipewa jina Palmerston, jina la waziri mashuhuri wa zamani wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza na waziri mkuu karne ya kumi na tisa.
Kituo cha kuwanusuru wanyama, kimesema kwamba Palmerston, alikuwa mkakamavu na paka mwenye nguvu, ambaye haikuwa vigumu kwake kuwa na marafiki -- au maadui, katika makao hayo yake mapya katika afisi ya wizara ya nchi za kigeni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni