Jumanne, 12 Aprili 2016

JUMBA REFU KULIKO BURJ KHALIFA KUJENGWA DUBAI


Kampuni moja nchini Dubai imetangaza mpango wa kujenga jumba litakalokuwa refu kushinda jumba refu zaidi duniani kwa sasa, jumba la Burj Khalifa.
Kampuni hiyo ya Emaar Properties, inayosaidiwa na serikali, haijasema jumba hilo jipya litakuwa na urefu gani lakini imesema tu kwamba litakuwa “refu kiasi” kushinda jumba la Burj Khalifa lililo na urefu wa mita 828 (2,717ft).
Mradi huo utakaogharimu $1bn (£710m) umeratibiwa kukamilika tayari kwa maonyesho ya kibiashara ya Dubai Expo ya 2020.

Litakuwa na nyumba za makazi, eneo la kubarizi kwenye paa na hoteli pia.
Mchoro wa jumba hilo umechorwa na Mhispania-Mswizi Santiago Calatrava Valls.
Jumba hilo halitasima kivyake kama ilivyo kawaida kwa majengo marefu duniani na badala yake litashikiliwa na nyaya na mapambo ya pembeni.
  Burj
Jumba la Burj Khalifa ni maarufu sana
Wadadisi wanasema hilo huenda likafanya jumba hilo kutatumbuliwa miongoni mwa majumba marefu duniani.
Jumba la Burj Khalifa linatarajiwa kupitwa na jumba la Kingdom Tower linalojengwa mjini Jeddah, Saudi Arabia ambalo linatarajiwa kuwa jengo refu zaidi duniani litakapomalizika kujengwa 2020.
Jengo hilo litakuwa na urefu wa kilomita moja (maili 0.6).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni