Kimbunga Harvey kilifika maeneo ya Marekani bara Ijumaa jioni na kusababisha mvua kubwa na upepo mkali.
Upepo wa kasi ya hadi 130mph (215 km/h) ulipiga maeneo ya pwani ya Texas.Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kuwahi kupiga maeneo ya Marekani bara katika kipindi cha miaka 13 na kimesababisha uharibifu mkubwa maeneo hayo.
Mji wa Rockport ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Magari na majumba yaliharibiwa katika uwanja wa ndege wa mji huo...

...sawa na ndege kadhaa ndogo.

Lakini uharibifu katika mji huo haukufikia uharibifu ulioshuhudiwa Rockport.
Tayari kumetoka mafuriko Galveston.
Asilimia 45 ya usafishaji wa mafuta Marekani hufanyika katika ghuba hiyo.
Tangi la mafuta liliharibiwa akribu na mji wa Seadrift, katika wilaya ya Calhoun.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni