Ijumaa, 17 Novemba 2017

Picha ya kuokolewa kwa chui yashinda tuzo

A leopard, perched on a bed in a well, looks up at its rescuers in July 2012

 Wanakijiji na walinzi walimuokoa chui huyo kwa kurusha ndani kitanda kwenye kisima Mnamo Julai 19, 2012, Anand Bora alipokea simu isiyo ya kawaida saa mbili asubuhi na kufahamishwa kwamba chui alikuwa amekwama kwenye kisima katika kijiji kimoja jimbo la Maharashtra, magharibi mwa India.
Bw Bora alikimbia kwenye kijiji hicho cha Bubali na kupiga picha operesheni ya zaidi ya saa tatu unusu ya walinzi wa msitu na wanakijiji wakijaribu kumuokoa chui asife maji kisimani.
Ni mwalimu lakini mpiga picha na alipiga picha za kipekee siku hiyo.
Katika moja ya picha hizo, chui huyo kuwa anaonekana akitazama juu kuwaangalia wale waliokuwa wanamuokoa.
Picha hizo ilishinda tuzo ya upigaji picha wa wanyamapori nchini India wiki iliyopita.
Ushindi wake umeibua maswali kuhusu yaliyojiri wakati wa uokoaji huo.
Picha hiyo ya miaka mitano iliyopita ni ya kipekee kwani mara nyingi wanyamapori hushambuliwa na kuuawa na wakazi.
"Chui huyo alipotazama juu, anaonekana kuhisi kwamba hatungemuumiza, kwamba tulikuwa tunajaribu kumuokoa," Bw Bora ameambia BBC.
 
A leopard was tranquilised and then pulled out of a well with a net in Nashik in December 2010
Chui mara nyingi hudungwa sindano ya kuwatuliza au kunaswa kwa kutumia nyavu na baadaye kuachiliwa huru porini, mfano huyu aliyeokolewa Nashik Desemba 2010
Maafisa wa msitu walipofika, wanakijiji waliwafahamisha kwamba chui huyo alikuwa ameogelea kisimani kwa saa 25 akijaribu kujizatiti asizame.
Mvua ilikuwa inanyesha na wanakijiji walichimba mitaro kuelekeza maji kisimani wakidhania chuo huo angeogelea iwapo kisima kingejaa.
"Tuliwaambia angekuwa amekufa maji kufikia wakati huo," afisa mkuu mlinzi wa msitu Suresh Wadekar amesema.
Badala yake, Wadekar anasema aliamua kwamba chui huyo alihitaji kupumzika kwani alikuwa anapumua kwa nguvu.

Akisaidiwa na wanakijiji, walirusha matairi mawili yaliyofungwa kwenye vipande vya mbao na chui huyo akapumzika juu yake,.
Kisha walirusha kitanda ambacho walikuwa wamekifunga kwa kamba na chui huyo aliruka na kuketi kitandani.
Walimuinua mnyama huyo hadi juu.
"Chui huyo alipofika juu, aliruka mbio na kutorokea msituni. Yote yalifanyika kwa muda mfupi sana," anasema Bw Bora.

Wezi waiba mtambo wa ATM Nairobi, Kenya

Benki ya Equity

Benki ya Equity, Kenya
Polisi nchini Kenya katika jiji kuu Nairobi wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana na wizi mwishoni mwa wiki ambapo wezi walitoweka na mtambo wa kutoa pesa, ATM.
Wezi hao walitoweka na kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kwa sasa wakati wa wizi huo Jumamosi.
Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani.
Washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza wizi huo.
Akizungumza na BBC, kamanda wa jimbo la Nairobi Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma.
Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata umaarifa utadhani wanaiga filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni wizi wa benki unazidi kubadilika sana.
Mwaka uliopita, wezi waliojifanya wakaguzi wa hesabu katika benki hiyo walitoweka na dola za Marekani 300,000.
na

Jumatano, 15 Novemba 2017

Wezi wachimba njia ya chini kwa chini na kuiba pesa kwenye benki India

 A view inside the 25ft tunnel that the thieves dug

 Wezi walichimba njia hiyo kwa miezi kadha
Wezi katika mji wa Mumbai magharibi mwa India walitekeleza wizi kwenye benki moja inayomilikiwa na serikali baada ya kuchimba njia ya chini kwa chini ya urefu wa futi 25 (mita 8).
Walichimba njia hiyo kwa miezi kadha.
Polisi wameambia BBC kwamba pesa taslimu pamoja na vito vya thamani isiyojulikana viliibiwa.
Maafisa wanaamini kwamba wezi hao walikodisha chumba karibu na Benki ya Baroda kuwawezesha kuchimba njia hiyo.
Wanadaiwa kuendesha biashara ya kuuza mboga na matunda katika kiduka chao kuficha mipango yao.
Wezi hao walitoweka tangu Jumamosi usiku baada ya kutokea kwa wizi huo.
  Polisi wanaamini wezi hao walikodisha duka karibu na benki hiyo
Polisi wanaamini wezi hao walikodisha duka karibu na benki hiyo
Haijabainika ni vipi wanaume hao walifanikiwa kuchimba njia hiyo kwa miezi kadha bila kugunduliwa.
Vyombo vya habari nchini India vimezungumza na wateja wa benki hiyo ambao vitu vyao vya thamani viliibiwa.
"Akiba yangu yote ilikuwa imewekwa kwenye sefu. Vito ambavyo tumemiliki kwa vizazi kadha, vimeibiwa," Dagdu Gavani, mmoja wa wateja aliambia Mumbai Mirror.
Wafanyakazi wa benki hiyo iliyo viungani mwa mji wa Mumbai waligundua wizi huo Jumatatu na kuwafahamisha polisi.

Polisi wameambia BBC kwamba sefu 30 kati ya 225 kwenye benki hiyo ziliporwa.
Washukiwa bado hawajatambuliwa.
 
Benki ya Baroda humilikiwa na serikali
Benki ya Baroda humilikiwa na serikali

Jeshi la Zimbabwe Lawatia Mbaroni Mawaziri Watatu wa Mugabe

SeeBait
Mawaziri kadhaa katika serikali ya Rais Robert Mugabe wamekamatwa baada ya Jeshi la Ulinzi kuonyesha uwezo wake na kushikilia majengo yakiwemo ya shirika la utangazaji (ZBC).

Milipuko mikubwa ilisikika na ikafuatiwa na ya bunduki katika maeneo yanayokaliwa na watu maarufu ya Borrowdale usiku kucha hali iliyozidisha hofu kwamba jeshi lilikuwa kazini.

Shirika la TimesLIVE limeripoti kwamba waliokamatwa ni watu maarufu kutoka kundi la G40 ndani ya chama cha Zanu PF lililokuwa likiongozwa na memsapu wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.

Baadhi ya watu waliokamatwa ni Waziri wa Elimu Jonathan Moyo‚ Serikali za Mitaa Saviour Kasukuwere na Waziri wa Fedha Ignatius Chombo.

Jeshi limesema katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake moja kwa moja kupitia ZBC kwamba Rais Mugabe yuko “salama na mwenye afya njema”. Taarifa hii imekuja baada ya askari wakiwa na silaha jana Jumanne kwenda katikati ya mji wakiwa kwenye magari ya kijeshi.

Shirika la Utangazaji la Zimbabwe ambalo majengo yake yako eneo la Pocket Hills jijini Harare lilitekwa saa 10:00 alfajiri.

Soma: Jeshi lasema Mugabe, familia wako salama

Msemaji wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alitangaza kwamba jeshi lilikuwa linadhibiti kwa lengo la kuhakikisha linawashughulikia “wahalifu” wanaomzunguka Mugabe.

“Sisi tunawalenga wahalifu wanaomzunguka yeye (Mugabe) wanaofanya uhalifu ambao unawasababishia watu mateso katika Nyanja za kijamii na kiuchumi hapa nchini na kisha tutawafikisha kwenye vyombo vya sheria‚” alisema Moyo.

Magufuli aaigiza kubomolewa kwa jengo la shirika la kuzalisha Umeme,Tanesco.

Makao makuu ya shirika la kuzalisha na kusambaza umeme, TANESCO

Jengo la Makao makuu ya shirika la kuzalisha na kusambaza umeme, TANESCO Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara katika eneo la Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli ameagiza sehemu ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.
Jengo lingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.
Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.
Zoezi la bomoa boma limekuwa likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayodaiwa kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.
CHANZO: BBC

Jumanne, 14 Novemba 2017

Bwana harusi apigwa risasi ya nyeti Misri

Ufyatuaji wa risasi kusherehekea swala fulani katika eneo la mashiriki ya kati ni kitu cha kawaida

Ufyatuaji wa risasi kusherehekea swala fulani katika eneo la mashiriki ya kati ni kitu cha kawaida

Bwana harusi moja nchini Misri amejeruhuwa vibaya baada kupigwa na risasi iliokuwa imefyatuliwa ili kusherehekea harusi yake.
Bwana harusi huyo alipata majeraha mabaya katika sehemu yake ya siri , nyongani na mkononi na anatibiwa hospitalini.
Osman al-Alsaied mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisherehekea usiku wake wa mwisho akiwa kapera wakati silaha hiyo ilipofyutuliwa upande wake badala ya hewani.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa kiuzembe na mwananume mwenye umri wa miaka 26.

Wanasema kuwa alitoroka muda mfupi baadaye baada ya kisa hicho lakini akakamatwa na sasa anahojiwa.
Ripoti za kisa hicho zimechochea hisia kali katika mtandao wa kijamii huku wengi wakitaka sherehe ya kufyatua risasi hewani kusitishwa.
 
Sherehe za harusi nchini Misri hupendwa sana
Sherehe za harusi nchini Misri hupendwa sana
Iwapo unafyatua risasi wakati unasherehekea furaha yako je itakuwaje wakati unapokasirika, ujumbe mmoja wa Twitter uliuliza.
Kulikuwa na kisa kama hicho katika harusi nchini Misri mwezi uliopita kulingana na mtandao wa Stepfeed.
Katika kisa hicho bwana harusi alifanyiwa upasuaji na matibabu baada ya risasi kumpiga katika nyonga yake

Mahakama yasikiza kesi inayopinga uchaguzi wa Uhuru Kenyatta: Hukumu tarehe 21.11

Mahakama ya juu nchini Kenya inasikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta

Mahakama ya juu nchini Kenya inasikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Uhuru Kenyatta
Kwa mara ya pili katika chini ya kipindi cha miezi mitatu, macho yote sasa yanaangazia mahakama ya upeo wa juu zaidi Kenya, itakayoamua iwapo ushindi wa rais Kenyatta, ni halali au la.
Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Kenya na tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya uchaguzi wa marudio ya Oktoba 26.
Kesi tatu zimewasilishwa mbele ya majaji 6 wanaoongozwa na jaji mkuu David Maraga, mbili zikitaka ushindi wa rais Kenyatta ubatilishwe, huku moja ikitaka viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga wachukuliwe hatua kwa madai ya kuchochea wafuasi wao kususia uchaguzi, na kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
 Rais Uhuru Kenyatta
 Rais Uhuru Kenyatta Kesi za kubatilisha ushindi wa rais Kenyatta zimewasilishwa kwa misingi kwamba tume ya uchaguzi ilikosa kuagiza uteuzi mpya wa chama ufanyike baada ya mahakama ya upeo wa juu zaidi kufutilia mbali ushindi wa rais Kenyatta mwezi Agosti.
Mahakama ina chini ya siku saba kusikiliza na kuamua kesi hizo tatu.
  Kiongozi wa upinzani nchini humo alisusia uchaguzi huo
Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Amolo Odinga
Uamuzi rasmi unatarajiwa kutolewa tarehe 21 mwezi huu.

Mahausi Girl kutoka Tanzania: Wanavyoteswa Uarabuni

Wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wanadhulumiwa uarabuni

Wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wanadhulumiwa uarabuni Wafanyakazi wa kike wa nyumbani kutoka nchin Tanzania walio nchini Oman na milki ya nchi za kiarabu UAE, wanadhulumiwa kimwili na kingono, wakiwa wanafanya kazi masaa mengi na wakilipwa mishahara midogo, kwa mujibu wa shirika la kitetea haki za binadamu, Human Rights Watch (HRW).
Kwenye ripoti iliyotelewa leo, HRW ilisema kuwa kuna maelfu ya wafanyakazi wa nyumbani kutoka Tanzania wako nchini Oman na UAE.
Watafiti wake waliwahoji 50 kati yao na kugundua kuwa karibu wote walipokonywa pasipoti zao walipowasili na kulazimiswa kufanya kazi hadi masaa 21 kwa siku bila kupumzika.
Wafanyakazi waliotoroka waajiri dhalimu na maajenti walisema kuwa polisi au balozi zao ziliwalazimisha kurudi la sivyo wangekosa mishahara yao hali iliyowachukua muda mrefu kutafuta pesa za kuwawezesha kurudi nyumbani.
Walisema kuwa walilipwa pesa kidogo kuliko zile waliahidiwa, au walikosa kulipwa kabisa, wakalazimishwa kula chakula kulichooza au mabaki ya chakula na kutukanwa kila siku, na pia kudhulumiwa kingono.

Sweden yafuzu kombe la dunia 2018 Italia OUT

Mara ya mwisho Italia kushindwa kufuzu kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1958

 Mara ya mwisho Italia kushindwa kufuzu kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1958
Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden.
Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930.
  baada ya mchezo huo mlinza mlango wa muda mrefu Gianluigi Buffon ametangaza kustaafu soka la kimataifa
Baada ya mchezo huo mlinza mlango wa muda mrefu Gianluigi Buffon ametangaza kustaafu soka la kimataifa
Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.
Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.
Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao.
  Mara ya mwisho Sweden kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 2006
Wachezaji wa Sweden wakisherehekea kufzu.
 
Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao kwa upande wa Italia lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.
Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.

Rubani aliyeundia ndege juu ya nyumba yake India

Indian pilot Captain Amol Shivaji Yadav poses beside his self- constructed TAC-003 aircraft at The India Aviation 2016 airshow at Begumpet Airport in Hyderabad on March 16, 2016. Yadav, a pilot with Jet Airways, has manufactured the aircraft which has been certified by Hindustan Aeronautics Limited (HAL), at his home in the western Indian city of Mumbai. The fifth edition of India Aviation, a five day event scheduled to run from March 16-20, more than 200 exhibitors from 12 countries.

 Ndege ya Amol Yadav iliwekwa kwenye maonyesho mwezi mwaka uliopita Miaka saba iliyopita Amol Yadav alitangaza kwa familia yake na marafiki kuwa angejenga ndege juu ya nyumba yao katika mji wa Mumbai India.
Familia na marafiki waliokua wamepigwa na butwa walimuuliza rubani huyo ni vipi angeweza kuishukisha ndege ikikamilika
"Kwa uhakika sijui," aliwajibu.
Bw Yadav ni rubani wa ndege za kutumia injini mbili.

Walijikakamua kupandisha vifaa vya kuijengea ndege hiyo hadi paa la nyumba ya familia la ghorofa tano, ikiwemo injini iliyonunuliwa kutoka ng'ambo ya zaidi ya kilo 180.

  Plane built on the roof
Ilipokuwa ikijengwa juu ya paa la nyumba
Mwezi Februari mwaka uliopita, ndege hiyo ya injini moja yenye nafasi ya watu 6 ilikuwa imekamilika.
Kulingana na Bwa Yadavm, ndege hiyo ndiyo ya kwanza kujengewa nyumbani nchini India.

Anasema kuwa injini hiyo ina nguvu za kuiwezesha ndege hiyo kupaa umbali wa futi 13,000 na tanki lake linaweza kubeba mafuta ya kuiwezesha ndege hiyo kusafiri umbali wa kilomita 2000 kwa kasi ya kilomita 342 kwa saa.
Serikali ilikuwa imeandaa maonyesho ya vifaa vilivyotengenezwa chini India mji Mumbai.

 
Car with plane
Ikipelekwa kufanyiwa majaribio
Wakati Yadav aliomba ruhusa kutoka kwa waandalizi kuonyesha ndege yake, walikataa wakisema kuwa hakukuwa na nafasi ya kutosha. Ilibidi ndugu wake wang'ang'a kutafuta nasafi.
"Kwa hivyo tuliamua kuobomoa ndege hiyo ili tuishukishe kwa sehemu tofauti na tuipeleke kwa maonyesho kwa lazima na kuionyeha kwa dunia, Bw Yadav alisema.

Waliibomoa ndege na kutenganisha injini, mkia na mabawa na kuishukisha kwa kutumia kreni.
Sehemu hizo ziliwekwa kwenye lori na kusafirishwa huku sehemu nyingine ikivurutwa na gari ndogo umbali wa kilomita 25.

 
Ndege hiyo kwa sasa imeegeshwa katika uwanja wa ndege ya Mumbai
Waliruhusiwa kuingia kwa maonyesho ambapo yeye na mafundi wake waliiunganisha ndege hiyo kwa muda wa saa tatu.
Wakati maonyesho yalianza ndege hiyo iliwavutia watu wengi.
Gazeti moja liliandika taarifa hiyo hali iliyochangia wageni wengi kufika akiwemo waziri wa safari za ndege wa India na wafanyabiashara.

Bwana Yadav sasa anasema kuwa yuko tayari kujenga ndege ya kwanza kabisa kujengwa India.
Wawekezaji wameonyesha moyo wa kuwekeza na serikali ya BJP imeahidi kumpa ekari 157 za ardhi za kujenga kiwanda cha kuunda ndege za kubeba abiria 19.



 
Bw Yadav saa anajenga ndege yaabiria 19 juu ya  nyumba


Jumatatu, 13 Novemba 2017

Mahakama yamhukumu Lulu miaka 2 jela kwa kifo cha Kanumba

Muigizaji Elizabeth Michale, maarufu kama 'Lulu

Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu
Mahakama kuu ya Dar es salaam imemhukumu muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael, maarufu kama 'Lulu', kifungo cha miaka miwili baada ya kumtia hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.

Alhamisi, 9 Novemba 2017

Picha za tembo waliochomwa moto yashinda tuzo

Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.

 Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.
Picha za tembo wawili wanaoonekana wakiutoroka umati wa watu uliowachoma moto imeshinda tuzo kuu katika shindano la picha za wanyama pori.
Picha ya Biplab Hazra inaonyesha tembo mtoto akichomeka moto huku yeye na tembo mkubwa wakitoroka kwa kuhofia maisha yao mashariki mwa India.
Akitangaza tuzo hiyo, jarida la Sancuary lilisema kwamba unyanyansaji wa aina hii unafanyika mara kwa mara.
Picha hiyo ilichukuliwa magharibi mwa Bengal ambako migogoro kati ya wanyama na binaadamu imekithiri.
Haijulikani ni nini haswa kilichotokea kwa wanyama hao katika picha hiyo ilioshinda tuzo ambayo ilipigwa katika wilaya ya Bankura.
  Picha ya Tembo waliochomwa moto yashinda tuzo
Picha ya Tembo waliochomwa moto yashinda tuzo
Wilaya hiyo imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwa vifo vya binadamu vinavyotokana na mzozo na tembo.
Ujumbe huo ulisema ''Umati wa wanaume waliokuwa wakiwazomea tembo hao ulikuwa ukiwachoma'' wakati Biplab Hazra alipopiga picha hiyo.
Anakumbuka kelele za ndovu hao walipokuwa wakitoroka.
''Kwa wanyama hao wazuri ,wanaowavutia Jamii sasa wako katika hali ya mbaya'', aliongezea.
Picha hiyo imevutia wengi katika mitandao ya kijamii.
Mainak Mazumdar anayeishi Bankura, alisema kuwa wanakijiji ni wa kulaumiwa kwa kuharibu mazingira ya wanyama pori na kwamba tembo wamekuwa wakinyanyaswa ma kuteswa.
Lakini alisema tembo wamewatesa wanadamu kwa kuharibu mimea yao, mashamba na kuwaua wato wasio na hatia