Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara katika eneo la Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli ameagiza sehemu ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na kusambaza umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.
Jengo lingine ambalo litaathiriwa na agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.
Imeagizwa majengo hayo kubomolewa kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.
Zoezi la bomoa boma limekuwa likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam na maeneo mengine ya nchi yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayodaiwa kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.
CHANZO: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni