Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amehofiwa kufariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.
Wu
Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya
kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya
majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.
Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.
Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni