Wapenzi wiwili
nchini India wamekamatwa kwa kumuua mume wa mwanamke na kisha kujaribu
kumfanyia upasuaji wa kubadilisha sura mwanamume mpenzi ili aweze
kuchukua mahala pake,
Tindi kali ilimwagwa kwenye uso wa
mwanamume, mpenzi wa mwanamkea, katika shambulizi lililopangwa, huku
wapenzi hao wakipanga kusema kuwa sura yake ilikuwa imebadilika baada ya
upasuaji.Lakini ndugu wa bwana wa mwanamke aligundua mpango huo alipofika hospitalini.
Alitoa malalamiko yake kwa polisi ambao walifanya uchunguzi wa vidole na kugundua njama huyo.
Mke, Swati Reddy amekamatwa. Polisi waliiambia BBC kuwa watamkamata pia mpenzi wake, Rajesh Ajjakolu mara atakapotibiwa majeraha yake na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.
Bwana Sudhakar Reddy anadaiwa kuuliwa usiku wa tarehe 26 Novemba na mwili wake kutupwa siku iliyofuatia. Hadi sasa mwiwi huo bado haujapatikana.
Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo amekiri kuwa walimuua mume wake.
Rajeshi Ajjakolu alilazwa hospitalini tarehe 28 Novemba huku Bi Reddy akiwajulisha familia ya mume wake kuhusu shambulizi la tindi kali.
Polisi wanasema kuwa wazazi wa Bw. Reddy waliamini kuwa mwanamume ambaye alikuwa akipata matibabu alikuwa ni mtoto wao na kulipa hadi dola 7,758 kama bili ya hospitali.
Njama hiyo haikugunduliwa hadi tarehe 9 mwezi Disemba, wakati ndugu yake Reddy, alifika hospitalini humo na kuwajulisha polisi aliposhuku kuwa mwanamume huyo hakuwa ndugu yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni