Familia moja kutoka Zimbabwe wamefanya uwanja wa ndege mjini Bangkok kuwa makazi yao kwa karibu miezi mitatu.
Kwa
mujibu ya ofisi ya uhamiaji wa Thailand, watoto wanne wenye umri chini
ya miaka 11 na watu wazima wanne walifika jijini Bangkok mwezi wa Mei,
lakini walikataa kurudi Zimbabwe kwa misingi ya usalama wao.Taarifa yao iliibuka baada ya mfanyakazi wa uwanja wa ndege huo alipoweka picha katika mtandao wa kijamii wa Facebook, akimpatia mtoto wa kike Mwafrika, zawadi ya Krismasi.
Picha hio,ambayo imefutwa sasa, iliambatana na ujumbe wa Kanaruj Artt Pornsopit akisema kuwa familia hiyo ilikuwa ikiishi katika jengo hili kwa miezi mitatu kwa sababu ya "hali ya sintofahamu" nchini mwao.
Msemaji wa ofisi ya uhamiaji Pol Col Cherngron Rimphadee aliiambia BBC kuwa awali familia hiyo iliwasili nchini Thailand kama watalii. Walijaribu kupanda ndege kutoka mjini Bangkok mwezi Oktoba hadi mji wa Barcelona nchini Uhispania kwa kupitia Kieve nchini Ukraine.
Lakini walikatiliwa kuingia katika ndege kwa sababu ya kukosa vibali vya kuingia Uhispania.
Pamoja na hayo walishindwa kurudi tena na kuingia nchini Thailand sababu kibali chao cha mwanzo cha kitalii kilichowakubalia miezi mitano kilipitwa na wakati na ilibidi walipie faini kubwa.
Familia hiyo imekataa kurudi Zimbabwe ikisema wanahofia usalama wao baada ya vurugu iliyotokea Novemba iliyomwondoa madarakani rais Mugabe aliyedumu kwa miaka 37.
Hata hivyo, kwa sasa hamna taharuki yeyote inayoendelea nchini Zimbabwe, kwa baadhi nchini humo wameyashuku madai yao kuhofia usalama wao.
Kwa mujibu wa Col Rimphahdee familia hiyo imewasilisha maombi ya kuomba makazi kwa Umoja wa Mataifa, wakati wakihudumiwa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi.
Aliimabia idhaa ya BBC Thai kuwa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR , limeomba familia hiyo ibaki nchini Thailand wakati jitahada za kuwapeleka nchi nyingine zikifanyika.
Nchi ya Thailand haina sheria ya kuwapatia makazi wakimbizi au watafuta hifadhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni