Jumanne, 31 Desemba 2013
JUISI YA NYANYA TIBA USIYOIJUA KIAFYA, HUPUNGUZA KIWANGO CHA KUPATA SARATANI.
Hata hivyo, watafiti nchini Marekani 
wamebaini kuwa wanawake wanaokunywa juisi ya nyanya angalau mara moja kwa wiki, 
wanapunguza kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya 
matiti.
Kwa mfano, wanaeleza kuwa glasi moja ya 
nyanya kwa siku ina kiwango sahihi na cha kutosha cha madini ya Lycopene, ambazo 
ni kemikali za mimea zinazoaminika kuondoa kukua kwa 
saratani.
Madini ya Lycopene ndiyo yanayozipa nyanya 
rangi yake nyekundu na nyanya hizo zimeundwa zaidi ya vichocheo vyenye uwezo wa 
kuzuia saratani hiyo.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Rutgers 
nchini Marekani walipima, kiwango cha vichocheo kwa wanawake 70 wenye miaka 55 
na kuendelea ambao walitumia juisi ya nyanya kwa wiki kumi. Wanawake hao ambao 
wengi walikuwa wanene kupita kiasi na baadhi wenye dalili ya saratani, 
walipungua uzito na saratani ilikwisha.
Kwa kuwa nyanya ni tunda linalopatikana 
wakati wowote, tena jikoni kwako, ni vyema wanawake wakajenga mazoea ya 
kuzitumia kama mlo hata wasipotengeneza juisi.
Imeandaliwa na Florence Majani, 
MWANANCHI.
Jumatatu, 30 Desemba 2013
RAIS DKT. KIKWETE AMTEUA ERNEST MANGU KUWA IGP MPYA
TASWIRA YA HAFLA YA KUKABIDHI RASIMU YA PILI YA KATIBA
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete 
akilakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. Warioba 
mara baaada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee Hall kupokea Rasimu ya Pili 
ya Katiba. Kulia ni Mhe. Assaa 
Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya 
Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana 
na Mhe Assaa Rashid, Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya 
Katiba, 
 Rais Kikwete akisalimiana 
na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu huku Jaji Mkuu wa Tanzania Bara 
Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Muungano Mhe Anne Makinda na Spika 
wa Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho wakisubiri zamu zao
 Rais Kikwete akimuamkia 
 na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi
 Rais Kikwete akimuamkia 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Cleopa David Msuya
 Meza kuu
 Jukwaa kuu la 
pili
 Sehemu ya wajumbe wa Tume 
ya Mabadiliko ya Katiba
 Waziri Mkuu Mstaafu Dkt 
Salim Ahmed Salim akiwa na wajumbe wenzie wa Tume na maofisa wa 
serikali
 Dkt Asha Rose Migiro, Mama 
Amne Salim na Mama Warioba
 Sehemu ya wananchi 
walioshuhudia tukio hilo la kihistoria
 Wananchi wakiwa katika 
hafla hiyo
 Wananchi wakifuatilia 
hafla hiyo
 Watangazaji wa TBC wakiwa 
kazini kurusha live tukio hilo
 Baadhi ya wazee mashuhuri 
katika hafla hiyo. 
 Wadau 
mbalimbali
 Wadau katika hafla 
hiyo
 Sehemu ya viongozi wa 
vyama vya siasa
 Wadau wa 
habari 
 Wanasheria nguli, Mzee 
Mark Bomani na Profesa Issa Shivji wakiwa miongoni mwa wadau
 Balozi wa Jamhuri ya 
Kidemokrasia ya Kongo Mhe Alfani Mpango akijumuika na wadau
 Baadhi ya viongozi wa 
vyama vya siasa na mabalozi
 Wadau na maafisa wa 
serikali
 Maafisa wa ofisi wa 
Masajili wa vyama
 Wadau
 Wadau na maafisa 
mbalimbali
 Makatibu 
wakuu
 Mawaziri wa Serikali ya 
Mapinduzi ya Zanzibar
 Mawaziri wa Bara na 
Zanzibar
 Mawaziri, wabunge na 
maafisa wa serikali
 Sehemu ya mawaziri wa bara 
na wa Zanzibar
 Msajili wa vyama vya siasa 
Jaji Mutungi (wa tatu kushoto) akiwa ameketi na wabunge na viongozi wa vyama 
mbalimbali 
 Sehemu ya waliohudhuria 
hafla hiyo
 Meza kuu ikimsikiliza 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mhe. Joseph S. 
Warioba 
 Rais Kikwete akimkabidhi 
Sir George Kahama nakala ya Rasimu ya Pili ya Katiba
 Rais Kikwete akiwakabidhi 
Mzee Hassan Nassoro Moyo na Jenerali Sarakikya nakala ya Rasimu ya Pili ya 
Katiba
 Rais wa Zanzibar na 
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akisoma hotuba 
yake
 Rais Kikwete 
akihutubia
 Wabunge na wadau wengine 
wakifurahia hotuba ya Rais Kikwete
 Rais Kikwete, Rais wa 
Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali 
wakiwapongeza wajumbe wa Tume kwa kazi nzuri
 Picha ya pamoja ya 
viongozi wakuu na wajumbe wa Tume
 Picha ya pamoja ya 
viongozi wakuu, wajumbe wa tume 
 Viongozi wakuu, viongozi 
wa vyama vya siasa na wajumbe wa Tume
 Katibu Mkuu Kiongozi 
Balozi Ombeni Sefue akisalimiana na Mhe Tundu Lissu
 Wajumbe wa Tume ya 
Mabadiliko ya Katiba 
 Rais Kikwete akiongea na 
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na 
Mbunge wa Kuteuliwa Mhe James Mbatia
Nikiripoti kutoka hapa 
katika viwanja vya Karimjee ni mimi.... wa Mlimani TV.PICHA NA 
IKULU
Jisajili kwenye:
Maoni (Atom)
 

.jpg)















































