Jumanne, 31 Desemba 2013

JUISI YA NYANYA TIBA USIYOIJUA KIAFYA, HUPUNGUZA KIWANGO CHA KUPATA SARATANI.


http://drleonardcoldwell.com/wp-content/uploads/2013/12/Food_Drinks_Glass_of_tomato_juice.jpgWENGI wetu tunaifahamu nyanya kama kiungo kwenye mapishi yetu au hata kachumbari kwenye mlo.


Hata hivyo, watafiti nchini Marekani wamebaini kuwa wanawake wanaokunywa juisi ya nyanya angalau mara moja kwa wiki, wanapunguza kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya matiti.

Kwa mfano, wanaeleza kuwa glasi moja ya nyanya kwa siku ina kiwango sahihi na cha kutosha cha madini ya Lycopene, ambazo ni kemikali za mimea zinazoaminika kuondoa kukua kwa saratani.

Madini ya Lycopene ndiyo yanayozipa nyanya rangi yake nyekundu na nyanya hizo zimeundwa zaidi ya vichocheo vyenye uwezo wa kuzuia saratani hiyo.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Rutgers nchini Marekani walipima, kiwango cha vichocheo kwa wanawake 70 wenye miaka 55 na kuendelea ambao walitumia juisi ya nyanya kwa wiki kumi. Wanawake hao ambao wengi walikuwa wanene kupita kiasi na baadhi wenye dalili ya saratani, walipungua uzito na saratani ilikwisha.

Kwa kuwa nyanya ni tunda linalopatikana wakati wowote, tena jikoni kwako, ni vyema wanawake wakajenga mazoea ya kuzitumia kama mlo hata wasipotengeneza juisi.

Imeandaliwa na Florence Majani, MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni