Jumanne, 28 Januari 2014
RAIS KIKWETE ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILOSA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitua katika tuta la barabara ya kuelekea Turiani.
Mheshimiwa Rais jana alitembelea waathirika wa mafuriko wilaya za Kilosa, Mvomero na Gairo mkoani Morogoro.
Katika ziara hiyo alijionea mwenyewe jinsi mafuriko yalivyoharibu daraja la mto Mkundi na pia kuharibu nyumba katika vijiji vya Magole na Mateteni wilayani Kilosa.
Aidha aliwaasa waathirika kuwa watulivu kipindi hiki wakati serikali inaangalia ni nini cha kufanya. Pia aliwagiza JWTZ kuja kuhakikisha kuwa wanawajengea nyumba za muda wahanga wote waliokosa makazi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni