Kiongozi wa kundi la LRA Joseph Kony
Joseph Kony kiongozi wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA) la nchini Uganda, ameiandikia ujumbe serikali serikali ya nchi hiyo akiomba msamaha na maelewano ya amani kwa ajili ya kumaliza uasi nchini.
“Nataka kuwafahamisha watu wa Uganda kwamba, sisi wanachama wa kundi la (LRA) tumeungana pamoja kwa ajili ya kurejesha amani iliyokumbwa na vita vya muda mrefu na serikali ya Rais Museven.” Umesema ujumbe wa Kony. Kony ameongeza kuwa (hapa ninanukuu):
“Tupo tayari kwa ajili ya kuomba msamaha na kusamehe na pia kudumisha amani na kumaliza vita hivi vilivyoathiri nchi za eneo la Maziwa Makuu za Afrika.” (Mwisho wa kunukuu)
Mazungumzo kati ya serikali ya Uganda na kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA), yaliyokuwa yakiendelea mjini Juba, Sudan Kusini, yalikwama baada ya Joseph Konyi kukataa kutia saini makubaliano ya mwisho mwaka 2008.
Joseph Konyi kiongozi wa kundi hilo la waasi wa (LRA) anaaminika kujificha katika misitu kati ya nchi ya Kongo DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati. (PT)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni