ASKARI POLISI WATANO WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA USIKU KWA KUGONGANA NA BASI DODOMA.
Ajali mbaya ya kusikitisha imetokea Jana usiku majira ya
saa nane ambapo gari ya ya polisi iliyokuwa inatoka Dodoma kwenye sherehe ya
polisi iliyokuwa inafanyika katika ukumbi wa Mipango.
Gari
hiyo iliyokuwa imebeba polisi na ilikuwa inaelekea Kongwa imegongana na basi ya
Mohamedi katika eneo la Mitumba ambalo ni nje kidogo ya mji ambapo wanawake
wawili na wanaume wa tatu wamefariki papo hapo ambao wote ni Polisi. Hakuna aliyejeruhiwa kwenye basi la Mohamed Trans na dereva wake alikimbia baada ya ajali hiyo.
Waliofariki ni:
- D9084 D/CPL Adolf Meshack miaka 51 Mgogo
- F 6459 CPL Evarist Moses Bukombe miaka 34 kabila Muha
- H3783 PC Deogratius Patric Mahinyila miak 29 kabila Mgogo
- WP 10337 PC Jakline August Tesha miaka 22 kabila Mchaga
- WP 10382 PC Jema Jimmy Luvinga miak 20 kabila Mhehe
(TK)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni