Alhamisi, 13 Februari 2014

BABA AMUUA MWANAE KINYAMA KWA KUMBAMIZA BARABARANI

ONESTORY Mgaya (31) mkazi wa kijiji cha Madaba Wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Nesta Mgaya mwenye umri wa miezi saba kwa kumbamiza chini kwenye barabara ya lami.

Kamamnda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimenke amesema,tukio hilo limetokea Februari 9 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi eneo la kijiji cha Lilondo wilayani humo.

Amesema, inadaiwa siku ya tukio mtuhumiwa na mkewe Blesila Mponda (30) pamoja na mtoto wao Nesta walifunga safari kutoka Madaba kwenda Lilondo kumsalimia mama wa mtuhumiwa ambapo wakati wakiwa njiani kutoka nyumbani kwa mtuhumiwa wakielekea kituo cha mabasi Blesila aligundua kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao hivyo alilazimika kumwachia mtoto mtuhumiwa ili kwenda kuchukua kadi hiyo.

Amesema, mtuhumiwa akiwa amembeba mwanae kuelekea kituoni ghafla alianza kumbamiza huyo mtoto chini kwenye barabara ya lami akiwa amemshika miguu na kumpigiza kichwa chini ambapo wakati akiendelea kufanya unyama huo watu waliokuwa jirani walifika na kwenda kutoa msaada ambapo mtuhumiwa alikimbilia porini na kumwacha mtoto chini.

Amefafanua zaidi kuwa, inadaiwa wananchi walilazimika kumkimbiza mtoto huyo kwenye kituo cha afya cha Madaba na kutokana na kuumizwa vibaya kichwani alihamishiwa hospitali ya serikali ya Rufaa Songea ambapo alilazwa wodi ya majeruhi kwa matibabu na siku iliyofuata aliaga dunia.

Hata hivyo Kamanda Nsimenke ameeeleza kuwa mtuhumiwa alikamatwa siku hiyohiyo ya tukio na anatarajiwa kupelekwa kupimwa akili ili aweze kufunguliwa mashitaka. (TK)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni