__320x320_5215a08d900a5
NIC Bank Tanzania watapata kiasi cha shiling bilioni 8.5/- kama nyongeza ya mtaji kutoka kwa wanahisa ili kuongeza ufanisi katika shughuli za kibenki kama vile utoaji mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati (SMEs).
Ongezeko hilo la bilioni 8.5/- litatolewa kwa awamu mbili kutoka kwa wanahisa wa NIC Bank Kenya na tayari bilioni 5.8/- zimeshatolewa toka mwezi desemba 2013.
Vile vile kuna ongezeko la shilingi bilioni 2.7 kutoka kwa kundi la wanahisa kutoka NIC Tanzania ambapo kabla ya Juni 2014 watakuwa wameshamaliza kutoa kiasi chote kitachotakiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NIC Tanzania Pankaj Kansara alisema kuwa wameamua kuongeza mtaji ikiwa ni katika mikakati ya kuboresha huduma za kibenki na vile vile kuweza kutoa mikopo kwa ufanisi kwa wajasiliamali wadogo na wa kati.
Kansara alisema kuwa benki ya NIC Tanzania ni benki yenye kutoa fursa katika kukuza biashara, miundombinu ya miradi mbali mbali na kuboresha mifumo ya biashara ambapo imeweza kusaidia kuvutia uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja na kuchochea ukuaji wa wajasiliamali wa kati na wadogo.
“Mpango huu wa kuongeza mtaji wetu ni sahihi sana kwani utaweza kutuwezesha kuongeza mikopo kwa soko Tanzania katika kuongeza ufanisi na utowaji wa mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati na vile vile katika makundi, ” alisema
NIC Bank Tanzania imeongeza mtaji wake baada ya kutoka shilingi bilioni 30 kwa mwaka 2009 hadi bilioni 180 / – mwaka 2013, ambapo ni asilimia 43 ya pato la ukuaji wa mtaji.
“Kwa kuangalia mafanikio ya benki yetu mama, tuna matumaini ya kuongeza nguvu na juhudi katika kuhakikisha kuwa tunatumia rasilimali zilizopo katika benki mama ya NIC Kenya kuendeleza na kukuza miradi mbali mbali ya maendeleo nchini Tanzania”
Aliongeza: ” NIC Bank Tanzania kwa sasa ina matawi katika mikoa ya Dar es Salaam , Arusha, Mwanza na Kahama ambapo kwa matawi haya tutaweza kusambaza huduma nyingi za kibenki na kuweza kuwafikia watu wengi ambao ni wahitaji”
NIC Bank Tanzania ni kampuni tanzu ya Nairobi Securities Exchange (NSE) ambao wapo na NIC Bank ambao wanamiliki hisa kubwa toka mwaka 2009