Mtuhumiwa Dorah Joseph (34). |
Kwa mujibu wa majirani na mashuhuda, kisa cha mwanamke huyo kufanya kitendo hicho cha kikatili, ni katika harakati zake za kutaka kumtumia mtoto huyo kishirikina ili aweze kujipatia mali.
Akizungumza muda mfupi baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Eleray alisema shangazi yake huyo amekuwa akimfanyia ukatili wa kutisha akishirikiana na jirani yake ambaye jina lake linahifadhiwa.
Happy alisema wazazi wake wote walishafariki, hivyo kumfanya yeye na dada yake kuishi kwa shangazi yake huyo, aliyemwelezea kama amekuwa akimtesa kwa kumnyima chakula, kumpiga, kumfunga mnyororo na kumfungia ndani kama mbwa.ANGALIA PICHA ZAIDI
Mtoto Happy Joseph (13).
‘’Shangazi ananitesa sana, ananifunga mnyororo kama mbwa na kunifungia chumbani, hanipi chakula wala kunipeleka shule, nina zaidi ya mwaka sasa sijaenda,” alidai Happy.
Aliongeza kuwa tofauti na dada yake, yeye ndiye amekuwa akiteswa huku ndugu zake wakizuiwa kumuona.
Akizungumzia tukio hilo, Askari wa Dawati la Jinsia, Deborah alisema ukatili uliofanywa na dada huyo kwa mwanafunzi huyo hauelezeki na kwamba wanakamilisha mashtaka ili kumfikisha mahakamani ili liwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye hadi anafikishwa polisi, alikuwa bado na mnyororo mguuni kutokana na kukosekekana kwa ufunguo wa kufungua kufuli kubwa mguuni kwake.
Kwa upande wake, mtuhumiwa huyo alisema alilazimika kumfunga mnyororo binti huyo baada ya kuchoshwa na tabia yake ya kuzurura ovyo, kwani muda mwingi anatoroka nyumbani na kwenda kusikojulikana.
Alisema mara kadhaa mtoto huyo amekuwa akitoweka nyumbani hapo wakati mwingine kwa wiki nzima bila kujulikana alikoelekea, ikiwa ni pamoja na kutoroka shuleni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni