Magari zaidi ya 3000 yamekwama eneo la Hedaru baada ya barabara kufungwa na kuzibwa na maji mengi yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha eneo hilo.Wasafiri wamekwama eneo hili kwani magari na mabasi pia magari ya mizigo yanashindwa kupita kwa kuwa barabara haionekani.
Kampuni ya ujenzi inayojenga barabara hiyo inajitahidi kuchimba maeneo ya pembeni ili kuweza kuhamisha maji ili angalau njia iweze kuonekana.Hali ni mbaya eneo hili hivyo serikali inatakiwa kuwahi kwenda kutoa msaada wa kuweza kupunguza maji na hatimaye magari yaweze kupita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni