Algeria imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia kuuawa kwa watu sabini na saba kwenye ajali iliyohusiha ndege moja ya Kijeshi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Abiria mmoja alinusurika ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Hercules C-130 iliyoanguka katika eneo la milima ya Oum al-Bouaghi, ikiwa njiani kuelekea mji wa Constantine.
Ripoti zinasema hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hiyo ya ndege.
Rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika amewasifu wanajeshi waliopoteza maisha yao na kuwataja kama wafia dini wa taifa hilo.
Wengi wa abiria sabini na nane waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa ni maafisa wa kijeshi na familia zao (TK).
Mabaki ya ndege ya jeshi la Algeria iliyoanguka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni