Mradi huo mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na upungufu mkubwa wa maji mjini Karatu unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Jijini Arusha (AUWSA). Pia, Prof. Maghembe alitembelea Halmashauri ya Mji wa Karatu kuangalia hali ya upatikanaji wa maji na utekelezaji wa miradi ya maji wilayani humo katika programu ya vijiji 10 ya BRN.
Miundombinu ya mradi wa maji wa dharura Karatu MjiniWaziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akiangalia tanki la maji la mradi wa dharura wa Karatu Mjini, huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya.Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akiangalia tanki la maji la mradi wa dharura wa Karatu Mjini, huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa AUWSA, Inj. Ruth Koya.Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Karatu Mjini.Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Felix Ntibenda (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Moses Mabula.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni