Samuel Eto'o akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya nne Uwanja wa Stamford Bridge
Hilo lilikuwa bao la 30 la Mwafrika huyo tishio kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya
Cahill akiifungia Chelsea na kukamilisha ushindi wa 2-0
Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea ushindi
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba akiingia Uwanja wa Stamford Bridge na timu yake ya Galatasaray
Drogba akikumbatiana na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kabla ya mechi
Baongo la kumpa heshima yake Drogba likiwa limetungikwa Stamford Bridge wakati wa mechi
CHELSEA itaendelea kupeperusha bendera ya England kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya usiku huu kuitoa Galatasaray ya Uturuki kwa jumla ya mabao 3-1 Uwanja wa Stamford Bridge, London kufuatia ushindi wao wa jana wa goli 2-0. Ikumbukwe kuwa mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Uturuki timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1.
Baada ya kutolewa kwa Manchester City na Arsenal katikati ya wiki iliyopita, Chelsea imejikatia tiketi ya kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga mabao 2-0 timu hiyo ya mchezaji wao wa zamani nyota, Didier Drogba.
Mabao ya Chelsea yamefungwa Samuel Eto'o dakika ya nne na Gary Cahil dakika ya 43.
Katika mchezo mwingine usiku huu, Real Madrid imeifunga Schalke 04 ya Ujerumani mabao 3-1 Uwanja wa Santiago Bernabeu na kuwatoa Wajerumani hao kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya awali kushinda 6-1 ugenini. Mabao ya Real yalifungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 21 na 74 na lingine Alvaro Morata dakika ya 75, wakati la Schalke limefungwa na Tim Hoogland dakika ya 31
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni