Mkurugenzi Mtendaji wa TV1 Tanzania, Marcus Adolfsson akizungumza na waandishi wa habari katika Hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam leo hii wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo kipya cha runinga kijulikanacho kama TV1, ambacho kitakuwa kikirusha matangazo yake kutoka jijini Dar es salaam na kuonekana nchini kote kupitia king`amuzi cha Startimes katika Channel namba 103 kwa mwonekano ulio bora kabisa.Mr. Adolfsson amesema TV 1 imekuja kuleta mapinduzi katika tasnia ya utangazaji wa runinga nchini Tanzania kwani vipindi vyake vya burudani na habari ni bora na vinatengenezwa kwa kumgusa Mtanzania wa hali ya chini.
Kidoti alisema Shoo hiyo itakuwa inaruka mara nne kwa wiki na itakuwa ikitayarishwa kwa ubora wa hali ya juu.
Pia aliongeza kuwa watakuwa wanafanya mahojiano na watu maarufu ili kuelezea uhalisia wa maisha yao juu ya mambo mbalimbali.
Sikaonga alisema taarifa yao ni tofauti na runinga nyingine kwani wamejikita kugusa maisha ya Mtanzania wa hali ya Chini.
Sikaonga alifafanua kuwa wanakusudia kuwa na wawakilishi wa TV I Mikoa yote na mpaka sasa wameshapata ripota mmoja jijini Mbeya, Bwana Laudence Simkonda Galimoshi.
Pia alisema wanajiandaa kutafuta mkarimani wa taarifa ya habari kwa watu wenye mahitaji maalumu ambapo alisisitiza kuwa mwishoni mwa mwezi huu watakuwa wameshampata mtu huyo ili taarifa ya habari ya TV1 iguse watu wote.
Nzowa alienda mbali zaidi kwa kusema amekaa muda mrefu katika fani ya Utangazaji, hivyo itakuwa rahisi kwakwe kutangaza habari bora kabisa kuwahi kutokea.
Msimamizi wa vipindi TV1, Irene Stanley akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo aliwaomba Watanzani kuitazama TV1 kwani ni kituo pekee cha runing ambacho kimejipanga kukata kiu ya mtazamaji katika habari na burudani.

Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliokuwepo katika uzinduzi huo.
Picha zote na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni