Glenn Ford
Mwanamume mmoja aliyeishi jela kwa zaidi ya miaka 25 akisubiri hukumu ya kifo nchini Marekani, ameachiliwa huru baada ya mahakama kubatilisha uamuzi wa mahakama kuwa alikuwa na hatia ya mauaji yaliyotokea mwaka 1983.
Glenn Ford, 64, alikuwa jela akisubiri hukumu ya kunyongwa tangu mwaka 1988 mwezi Agosti.
Mahakama wakati huo ilimpata na hatia ya mauaji ya Isadore Rozeman aliyekuwa na umri wa miaka 56 akiuza mikufu. Bwana Ford alikuwa mfanyakazi wake kwa wakati huo.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa Glenn ni mmoja wa wafungwa waliohukumiwa kifo kwa muda mrefu nchini humo na kuachiliwa.
Glenn alisema kuwa anahisi vizuri sana kwamba ameachiliwa.
Makosa kwenye kesi
Hakuna silaha yoyote ilipatikana na hapakuwa na mashahidi katika kesi hiyo.
Mwanamke aliyemhusisha Ford na mauaji hayo alisema kuwa ushahidi wake haukuwa wa kweli na kwamba alidanganya.
Mawakili wa Ford walioteuliwa na mahakama hawakuwahi kuendesha kesi ya mauaji
Bwana Mmarekani mweusi alihukumiwa na jopo la wazungu waliopendekeza auawe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni