Alhamisi, 20 Machi 2014

UTABIRI WA TB JOSHUA KUHUSU KUPATIKANA KWA NDEGE YA MALAYSIA WAANZA KUTIMIA



Wiki moja imepita tangu Mhubiri na Mtabiri mkubwa Nchini Nigeria TB Joshua alipotabiri kuwa Ndege ya Malaysia iliyopotea muda si mrefu wataipata ikiwa chini ya maji na wataanza kuona mabaki ya ndege yakielea juu ya maji ..Sasa leo habari mpya kuhusu ndege hiyo ni kuwa Huku Nchini Australia yameonekana mabaki ya ndege kwa njia ya Setelite ambayo bado yanafanyiwa uchunguzi kama ni ya ndege hiyo .

 

 

Waziri Mkuu wa Malaysia amethibitisha kuwa kumepepatikana uthibitisho wa ndege ya Malaysia Airlines flight MH370.

Setilait za Australia zimeona kitu kikielea kwenye bahari  ambacho kinaweza kuwa ndio mabaki ya ndege hiyo ambayo ilipotea toka tarehe 8/3/2014 ikiwa na abiria 239.

 

Msako mkubwa unaendelea leo katika sehemu hiyo mingawa kuna tatizo la upepo mkali pamoja na mvua kubwa inayonyesha. (TK)

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni