Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24, Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu za mdomoni, shingoni na paji la uso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamshna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.
Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.
Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote kujibu shitaka la kujaribu kujiua (TUKUO)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni